SABABU ZA UKE KUWA MKAVU..



(5)hivi uke kuwa mkavu inasababishwa na nini?
 
 *MAANA YA UKE* .
Uke (Vaginal orifice) ni uwazi uliochini ya urethra. Ni moja kati ya viungo vya uzazi vya Mwanamke. Uwazi huu unatofautiana katika muonekano na ukubwa kulingana na membrani nyembamba inayoitwa hymen.

 *KAZI ZA UKE*
☆Kupitisha damu ya hedhi.
☆Kuruhusu uume kufika sememu za ndani ya viungo vya uzazi vya mwanamke wakati wa kujamiana.
☆Kupokea shahawa wakati wa kujamiana.
☆Kupitisha mwili wa mtoto wakati wa kujifungua kwa njia ya kawaida (SVD).

 *SABABU ZA UKE KUWA MKAVU*
Ikimbukwe ni salama kwa uke kuwa mkavu katika mazingira yasiyo ya kujamiiana. Pia sio kiafya kwa uke kuwa mkavu wakati wa kujamiana na pia wakati mwingine huwa ni tatizo la kiafya.

♧Maandalizi yasiyotosheleza kabla ya kujamiana husababisha uke kuwa mkavu maana mwanamke anakuwa hayuko tayari kiakili kufanya tendo la kujamiiana.

♧Kukauka kwa uke katika umri wa 45+ huwa ni kiashiria cha ukomo wa hedhi kwa mwanamke. Lakini kama uke unakauka chini ya miaka 45 huwa ni tatizo la Afya ambalo huweza kuchangiwa na fangasi katika uke na kutokukaa sawa kwa homoni (hormonal imbalance) kwa mwanamke. Inashauriwa Mwanamke amuone Dactari kama ana tatizo hili ili apate ushauri zaidi, pia matumizi ya vilainishi kama K-Y jelly wakati wa kushiriki tendo la ndoa yameonyesha kusaidia katika hili tatizo.

♧Kutokuwa na hisia wakati wa tendo la ndoa pia kutokuwa na mapenzi na mwanaume unayeshiriki nayetendo la ndoa. Yote husababisha uke kuwa mkavu 

♧Ufanyaji wa tendo la ndoa kwa muda mrefu mfano masaa mawili. Pia msongo wa mawazo kwa Mwanamke na kutokuwa interested kiakili na kimazingira na tendo lile la ndoa. Pia ufanyaji mbovu wa tendo la ndoa mfano wanasema 'nje ndani nje ndani bila kuwepo na kuliwazana na kuwasiliana katika tendo la ndoa'. Yote hupelekea uke kuwa mkavu wakati wa tendo la ndoa.

Communicate for more questions...

Through:- kcmcsotz@gmail.com

Comments

  1. Njia gani itumike kwa mtu mwenye uke mkavu ili usiwe mkavu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante unknown, marejeo ya post ni salama uke kuwa mkavu ikiwa haujamiiani/ haushiriki tendo la ndoa. Ukiwa na uke mkavu wakati wa kushiriki tendo la mikiki mikiki inabidi urejee sababu za uke kuwa mkavu ambapo kikubwa ni maandalizi hafifu kabla ya tendo husika na kutokuwepo kwa hisia za mwanamke wakati wa mikikimikiki, au kufanya tendo kwa muda mrefu zaidi ya masaa mawili. Njia bora ni maandalizi mazuri, hisia na kufanya tendo kwa muda wa wastani sio zaidi ya masaa mawili.

      Delete
  2. Je uke ukiwa mkavu unauwezekano wakushika mimba kwel ingal ute wa mimba pia huupati nini kinasababisha ute wa mimba usitoke

    ReplyDelete
  3. Je endapo nakosa hisia za mapenzi na uke unakua mkavu wakati wa kishiriki tendo nifanye nini

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUPATA MTOTO WA KIUME

MISEMO HASI YA WAHENGA..