MISEMO HASI YA WAHENGA..
repost
*NABADILISHA MISEMO HII YA WAHENGA*
Barani Afrika kuna misemo mingi ya wahenga ambayo watu wengi sana hupenda kuitumia bila hata kufikiri sawa sawa. Kuna siku nilitafakari nikagundua hata enzi za wahenga walikuwepo wahenga wazembe na wavivu, walevi, wanga, watenda maovu na watenda mema na misemo walisema mingi ili kuhalalisha hali walizokuwa nazo.
Hivyo siyo kila msemo wa wahenga unabusara ndani yake. Siyo kila mzee unayemuona anabusara ndani yake maana hata wajinga nao wanazeeka. Usifirikiri mtu aliyekuwa na ujinga mwingi katika utu uzima wake anaweza akawa na busara nyingi akizeeka. Kuna wazee ukisikiliza ushauri wao unapotea fasta tu. Kwa mfano:
Msemo unaosema, “Mashika mawili moja humponyoka”, Huu msemo si sawa maana ni mhenga fulani ambaye alikuwa hawezi kufanya kitu zaidi ya kimoja kwa mara moja na akavifanyikisha vyote ndio alisema msemo huu kuhalalisha uwezo wake alionao.
Sasa kijana wa leo utasikia na yeye na uvivu wake anasema hivyo hivyo. Ngoja nikuoneshe kitu, Bilionea Mo anakampuni zaidi ya 40 ambazo kila siku zinafanya kazi na yeye anapokea ripoti za utendaji na kuziongoza nje ya familia na vitu vyake vingine alivyonavyo. Sasa wewe unashindwaje kuwa hata kiranja tu wakati unasoma kisa unaogopa kufeli?
Naufuta msemo huu leo kwako na kukupa uelewa mpya ya kwamba “Unaweza kushika hata mambo 20 kwa mara moja na lisikuponyoke hata moja”
Msemo mwingine ni ule unaosema, “Aliyekuwa juu mngoje chini”, Huu msemo nao ni wa kinafiki sana na unafanya vijana wengi wafikiri kuwa wale watu waliofanikiwa wawasubirie wakiwa wamefeli. Yaani kama leo hii ukae unasubiria mzee Reginald Mengi awe maskini ili uoneshe kwamba aliyekuwa juu mngoje chini.
Yaani hata Mungu hapendi hizi kejeli. Naubadilisha msemo huu kwako kuanzia leo, “Aliyekuwa juu mpandie huko huko maana ukimsubiria chini yeye anazidi kupanda wala hashuki”. Tuache kuwa tunawaombea watu mabaya kwa misemo ya wahenga isiyo na mashiko.
Msemo mwingine mbaya kabisa wa wahenga ni ule usemao, “Wambili havai moja” .Msemo huu unaweza ukachukuliwa kumaanisha kwa yeye aliyemaskini hawezi kuwa tajiri, Yeye anayefeli darasani hawezi hata siku moja akafaulu au yeye ambaye anatokea jamii fulani hawezi kufikia akawa mtu mkuu wa kuheshimika kwenye jamii fulani. Najiuliza mwenyewe kila siku hivi huyu mhenga alikuwa anawaza nini?
Naufuta msemo huu kwenye kizazi hiki na kuuandika msemo sahihi, “Uwe wa elfu moja, Uwe wa mia moja, Uwe wa kumi au wambili unaweza ukavaa moja, unaweza ukawa wa Kwanza, unaweza ukawa tajiri, unaweza ukawa mtu mkuu, unaweza kubadili hali ya jamii yako”
Sikiliza ndugu, vyovyote vile unavyotaka kuwa ukiamua kuchukua hatua UTAKUWA, achana na misemo hasi ya wahenga!

Comments
Post a Comment