USIOGOPE KUFANYA USALITI NA KUWAKIMBIA WATU HAWA
MARAFIKI WA KUWASALITI NA KUWAKIMBIA.
MARAFIKI 6 AMBAO UKIWASALITI UTAWEZA KUPIGA HATUA KATIKA JAMBO UNALOTAKA KUFANYA.
1. MADHARAU (CONTEMPT)
Huyu ni rafiki ambaye kila mda anakushauri kuwa wale watu ambao unadhani wanaweza kukusaidia kwa namna moja au nyingine hawana uwezo wowote wa kukusaidia. Kila mara anakutajia madhaifu yao, eti unamfuata fulani kwa kipi, kwa lipi analoweza kukusaidia ?.
Ukiweza kumsaliti na kuachana na huyu rafiki hakika utajenga msingi na marafiki wa faida kama vile heshima na kuweza kuthamini uwepo wa watu wengine kwamba wapo kwa ajili ya kukusaidia wewe.
2. ENEO LA FARAJA (COMFORT ZONE)
Huyu ni rafiki ambaye anajifanya kuwa ana huruma sana na wewe, kiasi kwamba hataki hata kukuona ukijaribu kufanya kitu kipya au kinaochonekana kuwa kigumu, kutisha, au hatari. Kila mara utasikia anakuambia achana nayo utaumia, utashindwa au utaabika.
Hakika ukiweza kumsaliti huyu rafiki pendwa, utajenga urafiki na watu kama vile ujasiri, udhubutu, na kujiamini, mwishowe utajikuta umepiga hatua kubwa sana katika safari ya kufukuzia ndoto yako.
3. UGHAIRISHAJI (PROCRASTINATION)
Huyu ni rafiki ambaye kila mara anapenda kukuweka busy na vitu vingine tofauti na mambo ya msingi unayotaka kukamilisha kwa wakati fulani. Kila mara unapofanya vitu vya msingi anakupangia ratiba nyingine isiyokuwa ya muhimu. Utasikia anakuambia umechoka bana, pumzika kwanza, au utafanya baadae, kesho au kesho kutwa.
Ukiweza kuvunja urafiki na ughairishaji, utajenga mahusiano na rafiki wa faida kama utunzaji wa mda, kufanya kwa wakati na mafanikio.
4. KUJISHUSHIA THAMANI (LACK OF SELF ESTEEM)
Huyu ni rafiki ambaye kila mara anakujengea sababu kadha wa kadha za kukufanya ujione hufai, huwezi lolote na hatimaye kukatisha tamaa na kujiona hauna thamani yeyote !
Ukikata mnyororo wa urafiki aina hii, utaweza kujijengea misingi imara ya kujiona wewe ni wa maana, kuna kusudi la kuishi kwako, na kutokukubali mtu yeyote akudharau.
5. KUJIFANYA (PRETENCE)
Huyu ni rafiki ambaye anapenda sana kukujaza upepo usiokuwa na faida wowote kwako, kila mara anakufanya ujione kuwa hakuna chochote usichokiweza. Hata kama kweli hujukijui kitu na unahitaji msaada, rafiki huyu atakuvimbisha kichwa na kuacha kutafuta msaada.
Ukiweza kuachana na rafiki huyu, utaweza kutambua mchango wa watu wengine katika kufanikiwa kwako, utaweza kujifunza pia vitu ambavyo hivijui na vyenye faida kubwa maishani mwako.
6. HOFU (FEAR)
Huyu bi rafiki ambaye anakuaminisha kwamba kufeli ni kitu kibaya sana, kiasi kwamba hauwezi hata kujaribu kufanya kitu unachokitaka kwa sababu ya kufeli. Mda mwingi anapenda kukujengea twasira ya kushindwa, kufeli na kuogopa kufanya jambo fulani.
# Ukimsaliti hofu kuanzia leo, hakika utafungua milango ya ujasiri, kujiamini na uwezo kujaribu kufanya jambo lolote la faida pasipo kuogopa kufeli. Utapata pia kufahamu kuwa kufeli sio mwisho bali ni ufunguo wa mafanikio mbeleni.
NOTE: Hauwezi kujenga tabia mpya pasipo kuvunja tabia nyingine. Ulivyo ni kwa sababu ya tabia ulizojijengea, ili uwe una gharama ya kutengeneza tabia mpya.

Comments
Post a Comment