USIOGOPE KUFANYA USALITI NA KUWAKIMBIA WATU HAWA
![Image](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjwg-PSTHbxZzh7EZS537BGRbKX8HW3h6EAie7KuDbSy7-BVWM8NnPKCMybZIcIaNitEu1KTJWIqWXZlc0PH6nLbHL9ldXLgx70qxx-DVHd8yiHqCcPbU2aLk4AU3yR2N_kHW4mz80bTSc6/s320/images-307.jpg)
MARAFIKI WA KUWASALITI NA KUWAKIMBIA. MARAFIKI 6 AMBAO UKIWASALITI UTAWEZA KUPIGA HATUA KATIKA JAMBO UNALOTAKA KUFANYA. 1. MADHARAU (CONTEMPT) Huyu ni rafiki ambaye kila mda anakushauri kuwa wale watu ambao unadhani wanaweza kukusaidia kwa namna moja au nyingine hawana uwezo wowote wa kukusaidia. Kila mara anakutajia madhaifu yao, eti unamfuata fulani kwa kipi, kwa lipi analoweza kukusaidia ?. Ukiweza kumsaliti na kuachana na huyu rafiki hakika utajenga msingi na marafiki wa faida kama vile heshima na kuweza kuthamini uwepo wa watu wengine kwamba wapo kwa ajili ya kukusaidia wewe. 2. ENEO LA FARAJA (COMFORT ZONE) Huyu ni rafiki ambaye anajifanya kuwa ana huruma sana na wewe, kiasi kwamba hataki hata kukuona ukijaribu kufanya kitu kipya au kinaochonekana kuwa kigumu, kutisha, au hatari. Kila mara utasikia anakuambia achana nayo utaumia, utashindwa au utaabika. Hakika ukiweza kumsaliti huyu rafiki pendwa, utajenga urafiki na watu kama vile ujasiri, udhubutu, na kujiamini, mwi...